Kama tunavyofahamu kwamba usb/USB port ina matumizi mbalimbali na ya msingi katika simu au kifaa chochote cha Electrinic.
Leo
tunaangalia njia za USB kwa simu ya Tecno F1.
Muonekano wa simu kwa nje
Kama una changamoto ya simu kusoma Njia za USB au Charging System na unataka kurekebisha njia hizo kwa njia rahisi na mkato yani Jampe, hii makala ni maalumu kwa ajili yako.
Utapaswa kuwa na usb yeyote ile yenye uwezo wa kuhamisha data, au usb yenye nyia nne ili kukamilisha zoezi la kufanya jamper haswa hama unataka ku flash simu kupitia computer.
Ukikata waya wa USB au Data Cable Ndani kuna waya nne za Rangi tofauti tofauti.
Mweusi
Huu ni waya maarufu kwa jina la Ground ambao ndo unasambaza Ground connection kwenye kifaa kizima na mara nyingi hugusishwa hata kwenye bati la sacket ya kifaa fulan.
Mwekundu
Huu ni waya wa 5V ama waya wa moto, ambao ndio hutoa moto iki kuwasha kifaa husika kama Vile kuchaji simu.
Mfano kwenye waya/usb unapoichomeka kwenye chaja au pc waya Mweusi (Ground) na Mwekundu zinatoa 5V.
Mweupe
Huu ni waya wa Signal au Data ambao unatumika kusafirisha Data na Signal kutoka kifaa kimoja kwenda kingine, na kwa kawaida waya huu unasafirisha Signal Hasi (-)
Kijani
Huu ni waya wa Signal au Data ambao unatumika kusafirisha Data na Signal kutoka kifaa kimoja kwenda kingine, na kwa kawaida waya huu unasafirisha Signal Chanya (+)
ZINGATIA
Kama tulivyojifunza kwamba katika USB waya Mweusi na Mwekundu kazi yake ni kupitisha chaji ya 5V ili Kuwasha power supply.
Mweupe na Mweusi kazi yake ni kuunganisha mawasiliano baina ya vifaa viwili vinavyosafirishiana Data Mfano Simu -Computer au Simu - Simu.
Au pindi unapotaka kuflashi simu kwa kutumia computer basi waya hizi za Data ndio husafirisha Taarifa au Command kutoka kwenye Computer kwenda kwenye Simu.
Njia hizi katika simu zimepewa majina mbalimbali ya utambuzi ili kuzilinganisha ili unapotaka kutumia njia mkato kama simu imeharibika Charge System au njia zake.
Majina
hayo ni kama ifuatavyo:-
GND -
Waya mweusi
VCN+ -
Waya mwekundu
DM -
Waya mweupe.
DP - Waya wa kijani.
Kwa
simu hii ya Tecno F1 Njia hizi zinapatikana Sehemu ya Chini Nyuma ya sehemu ya
System charge.
Kama unahitaji Njia kwa Ajili ya Chaji tuu bila data basi tumia
njia hizi mbili za Nyeusi (GND) na Nyekundu (VCHG+).
Ni matumaini yangu kwamba Makala hii imekupa elimu na umejifunza
usisahau ku Comment na kushare na marafiki.