MPENZI ROSEMARY SEHEMU YA 4

0

Story;MPENZI   ROSEMARRY. 
Mtunzi:jaffet jaka
MsAkaTongE OriJino
Sehemu ya 4:
KATIKA  muenderezo wa stori tutatumia jina la leah kwa sababu yote majina yake

Ilipoishia....
Piiiiii..! Ghafra nilisikia sauti ya breki ya Gari,
iliyosimama mbele yangu pindi naokota chungwa la
mwisho lililofika kabisa barabarani.
Nilibaki nimesimama kama shina la Uyoga huku
mikono yangu imeshika kichwa kwa woga.
Endelea.....
Ilikuwa ni gari aina ya NISSAN EXTAIR niliyowahi
kuiona ikiwa na mmoja wa wateja wangu wa
machungwa.
Alikuwa ni mrembo niliyemsaidia kubeba mfuko wa
machungwa siku anatoka Supermarket,kwenda
kwenye Gari hii.
Aliteremka na kunifuata pale nilipokuwa nimesimama
na kuniuliza " # MsAkaTongE_OriJinO kulikoni
tenaaaa??"
"Hahahahah" Kilikuwa ni kicheko cha yule mgambo
wa Jiji aliyebinua toroli langu mda mfupi uliopita.
"We Binti;Naomba umuache huyo Fukara aje atoe hiki
kimkokoteni chake hapa,huku akinipatia mauzo yake
yote kama Faini ya uchafuzi wa mazingira" Alisema
yule Mgambo.
Yule Mrembo alimtazama kwa dharau yule mgambo,
Akafyonza kwa nyodo kisha akatema mate chini.
Akamwambia "Shida yako Shilingi ngapi we Firauni
usiyekuwa na hata punje ya Ubinadamu??"
Kwa hasira yule dada alichukua pochi yake na kutoa
shilingi Elfu ishirini na kumpa yule Mgambo.
Ama kweli choo cha shimo Hakipigwi Air
Fresh...Kitanuka tu..!!
Yule mgambo alipokea ile pesa na akachukua
Machungwa mawili yaliyokuwepo pale chini na
kuondoka zake.
Niliumia sana kuona anazidi kuukata mtaji wangu.
Nilitamani kulia.
Yule dada alinisaidia kuosha machungwa yote
yaliyokuwa yamedondoka na kuyaweka katika toroli
langu.
Alienda mpaka lilipokuwa Gari lake na kulipaki
pembeni ya Barabara, ili kupisha magari yaliyokuwa
yakipiga honi kuomba njia katika baranara hii kubwa.
Alirudi mpaka nilipokuwepo na kunambia
"Pole sana ndugu yangu,Usijali kashfa za
Walimwengu.
Siku hizi Ubinadamu Mshumaa; Unawaka huku
unakwisha."
"Nilishazoea kukutana na Matatizo kama haya;
Daima MsAkaTongE Moyo napiga konde" Nilimjibu.
"Basi sawa Jemedari" Alinipa ujasiri.
"Utaanza kuuzia wapi baada ya kufukuzwa hapa??"
Itabidi nirudi nilipokuwa nauzia zamani,Stendi ya
Mabasi Ubungo. Nilimjibu kistarabu.
Aliniuliza kama nimekula, na akanipatia Elfu Arobaini
baada ya kutoridhishwa na Jibu langu.
Aliniomba aondoke,huku akiwa amenunua
machungwa mengi ya Juice.
Nilisita hata kuipokea pesa aliyonipa kulipia
machungwa kutokana na pesa lukuki alizokwishanipa
tia.
"Biashara haina Udugu,Ujamaa au Urafiki. Hii ni Pesa
ya biashara,pokea Tafadhali" Alisema huku
akiniwekea kwenye mfuko wa shati langu.
Shati hili nililipenda sana,sababu nililinunua kwa
biashara yangu ya nyanya nyumbani Morogoro.
Wakati Mrembo huyu anaondoka nilijipaka ujasiri wa
sabuni ndani ya maji,Nikamuita!.
"Dada Samahani.! Ningependa nifahamu Jina lako"
Ooooh! We unapenda ufahamu langu wakati we
ulishakataa kunipa lako!.?. Niliona haya kidogo.
"Ok fine,siku ukiwa tayari utanambia.! Mimi naitwa
Melan: MELAN PAUL KASANZU, alirudia kwa ufasaha
zaidi.
Bye Melan, Nimelipenda Jina lako.
Umefanana nalo kwa Uzuri: Nilichombeza kizushi.
"Mmmh! Yaani wewee! Sikuwezi": Alisema huku
akifungua mlango wa gari na kusepa.
***---***
Zilipita wiki mbili pasipo kufika kijiweni.
Nilikuwa hoi kitandani nikisumbuliwa na Maralia.
Mwili wangu wote ulidhoofu na kuishiwa
nguvu,kitendo kilichopelekea Machungwa yangu
kuoza yakiwa ndani tu.
Nilitumia pesa aliyonipatia Melan kununua baadhi ya
dawa za Maralia baada ya kulipa deni la Mama
mwenye Nyumba.
Mara nilisikia mlango wangu ukigongwa kutoka nje.
Nilijikongoja na kujivuta kivivu kuinuka mpaka
mlangoni.
Nilifungua mlango na kubaki nimeduwaa..! Ha.!
Melan????.
Alikuwa ni Melan akiwa ameambatana na Jamaa
yangu # Boy_Yogu .
Jamaa huyu ndiye aliyenipokea kijiweni na kunipa
wazo la kuuza Matunda.
Yeye pia alikuwa muuza Chipsi pale kijiweni.
Melan Alinikumbatia kwa furaha ya kuniona.
Oooooh! Best yangu,Nilikumisi: Alitamka kwa kubana
pua.
Nilijihisi mchafu kwa nguo Nyeupe ya Melan,ukizingat
ia nilikuwa Sijaoga siku ya pili leo kwa baridi la
Ugonjwa.
Sikuwa nanuka..!! Lakini Melan alinukia na kunifanya
nijihisi mchafu kwake.
Kwa wale waliosoma Saikolojia wanalijua vyema
suala hili la kujishtukia.
Niliwakaribisha Ndani Melan pamoja na Yogu.
Jamaa yangu alikataa na akadai hakuacha mtu
kijiweni.
Aliniletea tu mgeni wangu.
Baada ya Melan kuingia ndani, nilimwomba akae
kitandani maana sikuwa hata na Stuli ya wageni.
Nilikuwa na chumba kimoja tu, ambacho kilijazwa na
kitanda kidogo pamoja na beseni la vyombo.
Sikuhitaji chumba kikubwa kwani sikuwa na vitu vya
kunipa Gharama hiyo.
Melan alibaki kasimama tu, mpaka mimi nilipokaa
baada ya kumaliza kuufungua vizuri mlango ili
uingize hewa safi katika shimo hili.
Bila shaka hakuwa na Imani juu ya uimara wa
kitanda changu kilichopiga kelele za kuomba
Msamaha wa kuwekewa kitu kizito.
Kwichi kwichiiiiii....!! Kilitoa sauti ya Kusulubiwa na
Uzito wetu.
NB; TETELE KAINGIA TUNDUNI.???? ...Itaendeleiaah.
MsAkaTongE OriJinO.

Tags

Post a Comment

0Comments
Post a Comment (0)
To Top