
Imandikwa na SWAHIBU H JIRIWA Lushoto-Tanga.
Ni takribani wiki moja tangu tatizo la umeme lianze huko mkoani Tanga wilayani Lushoto. Umeme umekua ni tatizo kwa nyakati za mchana na unaporudi haustahamili hata kwa dakika 5, takribani muda wa wiki nzima sasa na bado linaendele. Wananchi wanaomba serikali iitume timu yake ya ufundi ili kuweza kutatua tatizo kwani linasabubisha kusimama kwa shughuli mbalimbali za kiuchumi. Mahitaji ya umeme ni jambo kubwa mno katika jamii kama vile eneo la Viti, kata ya shume kuna viwanda vya uchanaji wa mbao na zinatumika mitambo ya nishati ya umeme hivyo basi inabidi kusimama kwa kukosa umeme.
Maeneo yanayoathiliwa na kukosa umeme
- Mlalo
- Lukozi
- Malindi
- Viti
- Gologolo
- Manolo hadi maeneo ya Mambo
Kutokana na tatizo la umeme kituo cha umoja wa wakulima cha ukusanyaji wa maziwa Shume UWASHU kinagalimika kutumia Generator kwa masaa zaidi ya 16 ka kuwezesha mashine yakuhifadhia maziwa isigandishe maziwa jambo ambalo husababisha hasara kwenye kituo hicho.